1 Desemba 2012 - 20:30

Mufti Mkuu wa Saudia Arabia alisema kua maandamano tunayoshuhudia si ya Kiislam na ni hatari.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Sheikh Abdulaziz Ibn Abdullah Ali Sheikh Mufti Mkuu wa Saudia Arabia alisema: Maandamano ya kudai mahitaji ya Wananchi ni hatari na hayana faida isipokua ni shari.

Akieleza kunako mabadiliko na Muamko wa Kiislam katika nchi za Kiarabu na kudai kua maandamano hao hayana nsingo wowote ule yote ni kutaka maslahi binafsi tu.

Aidha alifumbia macho yanayotokea ndani ya Saudia Arabia kwa kuuawa watu wasokua na hatia huku akisema: Saudia kuna amani madhubuti na neema hii wengi waihitajia.

Mufti huyo wa Saudia Arabia alisahau nini wanachofanya wanajeshi wa Saudia ndani Bahrain na kuuwa Watoto wadogo huku akisema: Amani ya nchi itafutwe kwa silaha, kufanya hivyo Wananchi hawatoandamana tena dhidi ya Serikali kwa athari ya kipigo.

Maneno hayo ni baada ya kuandamana Wananchi wa Saudia Arabia katika Mji Mkuu Riadh kutaka kuachiwa wafungwa wa kisiasa nchini humo, na katika maandamano hayo watu kadhaa walijeruhiwa ambao ni Wanawake na Watoto walokuwa wakitaka waachiwe huru ayali na familia zao.